Jumapili 11 Oktoba 2026 - 17:20
Maandamano Makubwa Katikati ya Tokyo Yanayohusiana na Kuiunga Mkono Palestina

Hawza/ Katika kuadhimisha kumbukumbu ya operesheni ya “Tufani ya Al-Aqsa”, mamia ya waungaji mkono wa Palestina waliandamana katika mitaa ya mji mkuu wa Japani, Tokyo, wakitaka kukomeshwa ukaliaji wa ardhi za Palestina na kutetewa haki za wananchi wa Palestina.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, katika kuadhimisha kumbukumbu ya operesheni ya “Tufani ya Al-Aqsa” iliyofanywa na Harakati ya Hamas tarehe 7 Oktoba, pamoja na vita vya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina, idadi kubwa ya waungaji mkono wa Palestina na watu wanaotetea uhuru na haki walikusanyika katika eneo la Shibuya, lenye wakazi wengi, jijini Tokyo.

Washiriki wa mkusanyiko huo walitaka kukomeshwa ukaliaji wa kijeshi wa Israel katika ardhi za Palestina na kueleza mshikamano wao na wananchi wa Palestina.

Washiriki hao walibeba bendera kubwa za Palestina pamoja na mabango yaliyokuwa na kaulimbiu mbalimbali, zikiwemo “Palestina iwe huru” na “Komesheni mauaji ya kimbari.”

Aidha, waandamanaji walipaza sauti wakitaka kukomeshwa upanuzi wa makazi ya walowezi wa Israel na ukaliaji wa ardhi za Palestina, huku wakieleza uungaji mkono wao wa haki za Wapalestina.

Maandamano hayo yalipita katikati ya eneo la Shibuya na kufika katika makutano ya barabara ya Shibuya, ambayo ni miongoni mwa makutano yenye msongamano mkubwa zaidi jijini Tokyo, wakati wa saa za jioni ambapo watu wengi huwa wanatoka kazini.

Mandhari ya bendera za Palestina zikipeperushwa katika eneo la Shibuya, ambalo ni kitovu cha biashara chenye shughuli nyingi na mwanga mwingi, ilivutia hisia za wapita njia na watalii waliokuwapo katika eneo hilo.

Miongoni mwa kaulimbiu zilizopazwa na waandamanaji hao ni pamoja na: “Warudishieni Wapalestina ardhi yao,” “Walowezi waondoke,” “Ikomboeni Palestina, Ghaza na Ukingo wa Magharibi kuanzia Mto hadi Bahari,” na “Israel lazima ivunjwe na kusambaratishwa.”

Chanzo: Ava Press.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha